Wakati dirisha dogo la usajili msimu wa 2020/21 likifunguliwa rasmi leo Jumatano (Desemba 16), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Young Africans, Hersi Said, amethibitisha kamati yao imemepokea mapendekezo kutoka kwa kocha wao mkuu, Cedric Kaze, kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kuelekea mipango yao waliyojiwekea.

Young Africans wamedhamiria kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ambao kwa misimu mitatu mfululizo unashikiliwa na wapinzani wao Simba SC.

Hersi amesema maingizo mapya yanakuja na wanaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji mbalimbali ili kutekeleza mapendekezo hayo ya kocha.

“Kwa sasa tunaendelea na utaratibu huo wa kusajili na wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo kutokana na mapendekezo ya kocha, tukimaliza utaratibu huo tutaweka wazi tuliowasajili na wale wa kutolewa kwa mkopo,” amesema Hersi.

Hersi amesema Said Ntibazonkiza amekuwa wa kwanza katika usajili huo na kwa mujibu wa Kaze nyota huyo ataanza kucheza ligi hiyo, katika mechi yao dhidi ya Dodoma jiji FC Jumamosi wiki hii.

Wachezaji wanaotajwa huenda wakatolewa kwa mkopo Abdulaziz Makame, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Adeyum Salehe, Waziri Junior na Paul Godfrey.

Marekani : mshirika wa Trump ampongeza Biden
Lwandamina: Nitasajili dirisha dogo