Kocha Mkuu wa KMC FC Hitimana Thiery amelitaka Shirikisho la Soka Nchini Tanzania kuutazama upya Uwanja wa Nyankumbu unaotumiwa na Gaita Gold FC, ili kujiridhisha kwa mara nyingine, kama unafaa kutumika kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uwanja wa Nyankumbu umekua ukitumiwa na Geita Gold FC tangu ilipopanda Daraja misimu miwili iliyopita, lakini umekua hautumiki wakati wa Michezo ya Simba na Young Africans kwa hofu za kiusalama.

Hitimana amesema Uwanja huo hauna sifa za kutosha kutumika kwa ajili ya Michezo ya Ligi Kuu, na umekua tatizo kubwa kwa timu kadhaa kushindwa kucheza vizuri kwa kukosa viwango, huku wachezaji wakipata majeraha yasiyo ya lazima.

Amesema KMC FC imeshacheza Uwanjani hapo msimu huu na amejionea mazingira ya Uwanja huo ambao kwa mbali unaweza kuusifu ni Uwanja mzuri, lakini unapoukaribia ama kufika katika eneo la kuchezea ndipo utaona mapungu yake.

“Ningependa kuwataka viongozi wa TFF kuutazama upya Uwanja wa Nyankumbu unaotumiwa na Geita God FC, kiukweli ule Uwanja hauna sifa za kutumika kwa ajili ya Ligi Kuu, una mapungufu mengi sana katika eneo la kuchezea,”

“Ukiutazama kwenye TV ama ukiwa mbali kuanzia Mita 100 utausifia sana kwa kuona unakidhi vigezo vyote, lakini ukifika eneo la kuchezea, hali ni mbaya sana, ipo haja kwa viongozi wakajiridhisha tena.” amesema Kocha Hitimana

Young Africans yamnyima usingizi Allan Okello
Adebayor awakumbuka Mashabiki Simba SC