Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ublegiji, Marc Wilmots ametaja kikosi cha wachezaji 24, tayari kwa fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016), zitakazoanza mwezi ujao nchini Ufaransa.

Asilimia kubwa ya wachezaji waliotajwa na Wilmots, wanacheza soka katika ligi ya nchini England ambayo msimu wake wa 2015-16 itafikia kikomo mwishoni mwa juma hili.

Hata hivyo nahodha na beki wa Manchester City, Vincent Kompany ameachwa katika kikosi hicho, kufuatia maumivu wa paja yanayomkabili kwa sasa.

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard ni sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho sambamba na kiungo wa klabu ya Everton Kevin Mirallas.

Kikosi kamili kilichoitwa na kocha Marc Wilmots, upande wa makipa yupo Courtois, Gillet, Mignolet

Mabeki:

Alderweireld, Boyata, Denayer, Engels, Lombaerts, J. Lukaku, Meunier, Vermaelen, Vertonghen

Viungo:

Dembélé, Fellaini, Nainggolan, Witsel, Carrasco, De Bruyne, E. Hazard, Mertens

Washambuliaji:

Batshuayi, Benteke, R. Lukaku, Origi

Wachezaji ambao wameweka katika orodha ya tahadhari endapo changamoto yoyote itajitokeza wakati wote wa maandalizi ya fainali za Euro 2016 ni Chadli, Ciman, De Bock, G. Gillet, T. Hazard, Mirallas na Sels

Bocco Kuikosa African Sports
Diamond, Mafikizolo watua Bungeni

Comments

comments