Aliyekua Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza FC Mbwana Makata, huenda akajiunga na Klabu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Polisi Tanzania iliachana na Kocha kutoka nchini Burundi Joslin Bipfubusa mapema mwezi uliopita, kufuatia matokeo mabovu yaliyokiandama kikosi chao.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa Polisi Tanzania, zinaeleza kuwa wamepokea Wasifu mbalimbali wa Makocha wakihitaji kuifundisha timu yao katika kipindi hiki, lakini kwa sasa wanahitaji Kocha ambaye atawavusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

“Tulipokea CV (Wasifu) kutoka kwa makocha mbalimbali lakini kwa sasa tunayempendekeza na kumpa kipaumbele ni Mbwana Makata, kwa sababu ana uzoefu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,” amesema Kiongozi huyo

Makata anatajwa kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, kufuatia kosa la kuwaamuru wachezaji wa Mbeya Kwanza FC kugomea mchezo dhidi ya Namungo FC msimu uliopita 2021/22.

Korea Kaskazini kuandaa Fainali za Kombe la Dunia
Kocha Mbeya City aihofia Simba SC