Kocha Gerardo ‘Tata’ Martino ametangaza kuachana na Timu ya Taifa ya Mexico, baada ya kushindwa kuivusha hatua ya Makundi Kombe la Dunia 2022, zinazoendelea nchini QATAR.

Mexico ilianza kwa sare dhidi ya Poland kabla ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Argentina baadae ikaambulia ushindi dhidi ya Saudi Arabia katika Hatua ya Makundi, lakini imeshindwakufuzu Hatua ya 16 bora.

Mara ya mwisho Mexico kushindwa kutinga raundi ya 16 bora ilikuwa kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizounguruma nchini Argentina mwaka 1978.

Akizungumza baada ya kuachana na timu hiyo licha ya Mexico kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Saudi Arabia, Kocha huyo alisema “Ninahusika na matokeo haya mabovu, mkataba wangu umemalizika baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, hakuna kitu kingine cha kufanya baada ya hapa,”

Ushindi wa mabao 2-1 kwa upande wa kocha wa Mexico haukuwa na maana kwake kwani timu yake ilikuwa kataika hali mbaya baada ya kuboronga mechi zao za mwanzo dhidi ya poland na Argentina.

Tata aliteuliwa kuwa kocha wa Mexico tangu mwaka 2019 na Shirikisho la Soka Mexico, kabla ya kuinoa timu hiyo alikuwa na uzoefu wa kuzinoa timu nyingine za taifa za Uruguay na Argentina.

Aliwahi kuzipeleka Argentina na Uruguay kwenye fainali za Kombe la Copa America mwaka 2011, 2015 na 2016. Katika ngazi ya klabu Tite aliwahi kuzinoa Newell’s Old Boys, Barcelona na Atalanta United.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 2, 2022
Iptisam apata wastani 'A' mtihani darasa la saba