Licha ya Simba kuonekana kuwa ipo vizuri na ina mwenendo mzuri katika Ligi Kuu Bara msimu huu, kocha wa timu hiyo, Joseph Omog amesema kama wachezaji wake wasipokuwa makini basi Yanga itakuwa bingwa tena.

Simba ambayo  Jumapili hii inatarajia kucheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba sawa na timu zilizo juu yake ambazo ni Azam FC na Mbeya City lakini imezidiwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Omog ameyataja mambo hayo kuwa ni ubinafsi wa wachezaji, ukosefu wa umakini na uzalendo.

“Tunaonekana kama tupo vizuri na tumechanganya katika ligi, ukweli ni kwamba tusipokuwa makini katika mambo haya matatu ni lazima Yanga itwae ubingwa tena,” alisema Omog anayesaidiwa na Jackson Mayanja, raia wa Uganda.
Akizungumzia mchezo dhidi ya Mtibwa, Omog amesema: “Lengo letu ni lilelile, kuhakikisha tunapigana kila mechi japokuwa  najua haiwezi kuwa rahisi namna hiyo lakini tutapigana kadiri ya uwezo wetu ili tushinde.”

Wakuu wa Mikoa Kanda ya ziwa waeleza madhara ya tetemeko la ardhi lililoleta maafa
Show: Ruby alivyopendezesha shindano Miss Ilala 2016