Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans, huenda kikaongozwa na kocha kutoka DR Congo Mwinyi Zahera, katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Wekundu Wa Msimbazi Simba utakaochezwa mwishoni mwa juma hili uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Kocha Zahera ametua jijini Dar es salaam kwa ajili ya mipango ya kujiunga na young Africans, ambayo iliachwa solemba na George Lwandamina majuma mawili yaliyopita.

Baada ya kuwasili Dar es salaam, Zahera amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa “Master”, kwa muda wa takribani saa moja kabla ya kutembezwa sehemu kadhaa katika ofisi za klabu hiyo.

Kocha huyo alitarajiwa kuelekea mjini Morogoro ambako kikosi cha mabingw ahao wa Tanzania bara kimeweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Kocha Zahera alikuwa kwenye benchi la Ufundi la timu ya taifa ya DR Congo, The Leopard na ana uzoefu wa kufundisha soka hadi barani Ulaya, katika nchi ya Ufaransa.

Ngorongoro Heroes wapewa mapumziko
Wakazi Njombe waaswa kupima kansa ya kizazi na kuachana na imani potofu

Comments

comments