Klabu ya Horoya AC ya Guinea imethibitisha rasmi kuachana na Kocha Lamine N’diaye raia wa Senegal, baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Horoya AC walitaka kumuongezea mkataba Kocha Lamine N’diaye ili kuendelea kusalia katika klabu hiyo lakini kocha huyo alikataa kusaini mkataba mpya.

Nafasi ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 66 imechukuliwa na Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Guinea, Lappé Bangoura mwenye umri wa miaka 61.

Novemba 2019, N’diaye alitangazwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya Horoya AC akichukua nafasi ya Didier Gomes da Rose ambaye alifukuzwa kazi.

N’diaye anahusishwa na klabu ya Simba SC ya Tanzania, hii si mara ya kwanza kwa kocha huyo kuhusishwa na Klabu hiyo ya Msimbazi, kwani aliwahi kuhusishwa kujiunga na Mnyama kipindi alichoondoka kocha Didier Gomes da Rosa.

N’diaye amewahi kuwa kocha Mkuu wa Klabu za TP Mazembe-DR Congo (2010/11), AC Leopards-Congo Brazzaville (2013/14) na Al Hilal-Sudan (2018/19)

Mafanikio makubwa aliyowahi kuyapata kocha N’diaye

? 2010 – CAF Champions League – DR Congo (Tp Mazembe)
? 2010 – FIFA Club World Cup – DR Congo (Tp Mazembe)
? 2011 – CAF Super Cup ×2 – DR Congo (Tp Mazembe)
? 2019 – Ligue 1 Pro ×4 – Congo Brazzaville (AC Leopards)
? 2022 – Guinean Super Cup-Congo Brazzaville (AC Leopards)

Aliou Cissé afunga mjadala wa Sadio Mane
M23 Waendelea 'kuumiza vichwa' DRC