Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Rwanda ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Oktoba 14.

Kagere ameendelea kujifua na Simba ambapo mpaka jana hakuwa amepokea wito kutoka shirikisho la Soka nchini Rwanda.

Timu hiyo huenda ikatumia wachezaji wake wanaocheza ligi za ndani kama ilivyofanya Tanzania.

Kagere amesema anafahamu mchezo huo ni wa kirafiki hivyo hakuna cha kupoteza hata kama hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo.

“Timu yangu ya Rwanda itacheza na Tanzania, najua lakini kwa upande wangu sifahamu kama nitakuwa miongoni mwa kikosi hicho kwa kuwa bado sijaitwa, ngoja tusubiri, nikiitwa sawa, nisipoitwa pia haina shida,” amesema Kagere

“Sina wasiwasi sababu mchezo wenyewe ni wa kirafiki, hakuna cha kupoteza, inawezekana kocha ameamua kuwapa nafasi zaidi wachezaji wanaocheza ligi ya ndani.”

Utafiti wa visima vya mafuta waanza Tanzania
Tetesi za soka: Solskjaer akataliwa Manchester, Pulisic afikiriwa Chelsea