Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Sven Vandenbroeck amesisitiza kuitumia michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na KMC FC kama maandalizi ya kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya kwanza dhidi ya FC Platinum, utakaochezwa kati ya Desemba 22 na 23 nchini Zimbabwe.

Simba SC tayari wameshaelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa 15 dhidi ya Mbeya City, ambao utachezwa kesho Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Kocha Sven amesema muda uliosalia kuelekea mchezo dhidi ya FC Platnum ni mchache, hivyo hana budi kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi kuitumia michezo hiyo ya Ligi Kuu kama sehemu ya maandalizi.

Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji amethibitisha kuanza mipango ya mipango ya kuwafuatilia wapinzani wao FC Platnum, ili kutambua baadhi ya mbinua mbazo zitawasaidia kuwakabili kikamilifu katika michezo yote miwiwli itakayochezwa Bulawayo na Dar es salaam.

“Tuna siku chache kabla ya kukutana na Platinum ambazo ndani yake tunatakiwa kucheza mechi mbili za Ligi dhidi ya Mbeya City na KMC FC tumepanga kutumia michezo hiyo kuwa sehemu yetu ya maandalizi.” Amesema kocha Sven

Amesema amewaandaa wachezaji wake kwa upana wa kikosi alichonacho na kutakuwa na mabadiliko ndani yake kama walivyofanya katika mchezo na Polisi Tanzania ili hadi kufika siku ya mchezo dhidi ya FC Platinum awe na wachezaji walio tayari kwa mapambano.

“Lazima tuweke nguvu na nia thabiti ya kupata ushindi katika michezo hii miwili, malengo ya Simba msimu huu ni kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa maana hiyo tutakuwa tukiendelea kuwafuatilia Platinum katika maeneo ya kiufundi kama ambavyo tulifanya kwa Plateau United,” alisema.

Simba SC walitinga hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuiondosha Plateau United ya Nigeria kwa jumla ya bao moja kwa sifuri.

Mourinho, Bruno Fernandes watwaa tuzo England
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 12, 2020