Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania ’Taifa Stars’ Hemed Morocco ameahidi kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya DR Congo utakaochezwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari za michezo mapema leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar Es Salaam, Moroco amesema kikosi chake kimejipanga vyema kukabiliana na timu hiyo ili kupata ushindi katika mchezo huo utakaochezwa majira ya saa kumi jioni.

‘Itakuwa mechi nzuri na ngumu, tunaitaji kushinda ili kujiweka vizuri kwenye viwango vya FIFA’ Amesema Morroco.

Aidha, kocha huyo amesema kikosi cha stars kesho kitawakosa wachezaji wawili Abdulazizi Makame ambaye aliumia mazoezini lakini pia timu hiyo itaendelea kukosa huduma ya golikipa Aishi Manula ambaye hayupo vizuri kwa mchezo wa kesho.

Stars inaingia dimbani kucheza na DR Congo huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-1 siku chache zilizopita kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria.

Joe Gomez kuikosa Italia
EAEO: Idadi kubwa ya wahitimu vyuoni hawana sifa za kuajiriwa

Comments

comments