Kocha Mkuu Tanzania Prisons Mohamed Adolf Rishard amesema hesabu zake kubwa ni kuiwezesha klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi La Magereza Tanzania, kumaliza Ligi ikiwa ndani ya 10 bora msimu huu 2019/20.

Kocha Rishard ametoa kauli hiyo, zikisalia siku mbili kabla ya kuelekea kwenye mchezo wa mzunguuko wa 32 wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya mabingwa watetezi Simba SC, ambao kwa sasa wanaongoza msimamo wa Ligi hiyo kwa kufikisha alama 78.

Kocha huyo mzawa amesema, kikosi chake kinahitaji kufanya vizuri katika michezo iliyobakia, na ana uhakika mpango huo tafanikiwa kutokana na kuwa na kikosi kinachoundwa na vijana wa kazi.

“Tunahitaji kufanya vizuri mchezo wetu ujao na michezo mingine iliyosalia, tutakutana na timu nzuri na ngumu ila tupo tayari.” Amesema Rishard

Tanzania Prisons ipo nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi Kuu Tanzania bara kwa kufikisha alama 42, na tayari imeshashuka dimbani mara 31.

Keshokutwa Jumapili wataingia uwanja wa nyumbani (CCM Sokoine) wakiwa na mipango ya kujiongezea alama tatu muhimu dhidi ya Simba SC ambao pia wanahitaji matokeo mazuri, ili kulisogelea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Simba inahitaji pointi tatu ili kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo wanahitaji kuutwaa ubingwa wakiwa na michezo mingine mkononi.

JPM Arejesha Meli Bukoba, majaribio juni 28
Serikali yazitaka shule binafsi kupokea wanafunzi