Kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda, Johnny McKinstry amedai kuwa klabu pambano la Azam na Esperance ya Tunisia bado gumu sana kwa kuzingatia uzoefu wa Esperance katika michuano ya Afrika.

Hata hivyo kocha huyo kijana, ameongeza kuwa Azam wanaweza kuitupa nje ya mashindano Esperance endapo watafanikiwa kupata bao la ugenini.

“Esperance ni wazoefu katika ngazi hii. Pambano bado ni gumu sana hasa baada ya matokeo ya 2-1 hapa Tanzania. Lakini Azam wanaweza kwenda kujaribu na kumaliza kazi waliyoianza Nyumbani. Si jambo jepesi” McKinstry aliiambia Soka360 katika mahojiano na mtandao huu.

“Nadhani kama wanaweza kwenda na kupata bao la ugenini , nafikiri wanaweza kufuzu. Nadhani kwenda Tunisia na kujaribu kutafuta sare ya bila kufungana ni hatari sana”

Kama wanaweza kupata bao la ugenini watakuwa na nafasi kubwa mno ya kufuzu, siioni Azam wakiruhusu kufungwa mabao mawili au matatu.

Azam itakabiliana na Esperance katika mchezo wa marudiano Aprili 19, jijini Tunis katika pambano la marudiano linalotarajiwa kuchezeshwa na waamuzi wa Morocco kuanzia majira ya kumi na moja na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.

Ravia, Ali Mohammed Na Zam Ally Wakabidhiwa Soka La Zanzibar
Kocha Wa Twiga Stars Abebeshwa Jukumu Zito Zanzibar