Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba, ameasema kuwa kikosi chake kimewasili mkoani Shinyanga kwa lengo moja tu la kushinda mchezo dhidi ya Mwadui na kuzoa pointi zote tatu Jumamosi hii.

Kikosi cha Azam FC kiliwasili salama mkoani humo Jumatano kikitokea mkoani Dodoma, ambapo kwa mujibu wa ratiba ya kocha huyo wachezaji watafanya mazoezi mkoani humo kwa ajiri ya kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

“Wachezaji wote wapo tayari hakuna mchezaji majeruhi na morali ipo juu, wote tunaamini kama tutafanya kazi kama familia huku tukiweka tahadhali kwa wapinzani wetu, huwa nawaambia kuwa timu zote zinacheza mpira mzuri haijalishi ni Yanga ama timu yoyote, cha msingi ni kumuheshimu mpinzani na mchezo wenyewe, ninachohitaji ni ushindi siku ya Jumamosi na kupata pointi tatu,” amesema Cioaba.

Hata hivyo, mchezaji pekee ambaye ameshindwa kusafiri na kikosi hicho ni kiungo mkabaji Stephan Kingue, ambaye bado hajapona vizuri majeraha ya mgongo huku winga Joseph Kimwaga na mshambuliaji Shaaban Idd, wakiendelea na matibabu baada ya wote kufanyiwa upasuaji hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Ukimya wa Hamisa wazua minong'ono kwenye 40 ya pili ya Dee.
Halmashauri mkoani Tabora zatakiwa kuwatumia wanachuo

Comments

comments