Bosi wa kikosi cha Man Utd Jose Mourinho amechukizwa na hatua ya beki wake Eric Bailey kuitwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kwa ajili ya fainali za mataifa ya Afrika zitakazoanza baadae mwezi huu nchini Gabon.

Bailey alijumuishwa katika kikosi cha kwanza cha Man Utd wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Middlesbrough mwishoni mwa juma lililopita.

Jambo kubwa ambalo limemkera Mourinho ni hatua ya kocha wa kikosi cha Ivory Coast Michel Dussuyuer kumuhitaji Baily kabla ya Januari mbili, hali ambayo ilisababisha aukose mchezo wa jana dhidi ya West Ham Utd.

Tuliwaomba wamchukue tarehe 3 lakini wakakataa, hivyo ilikua sababu ya mchezaji huyu kukosa mchezo wetu na West Ham”. Alisema Mourinho.

Image result for Michel Dussuyuer and aric BaileyJose Mourinho akimpa maelekezo Eric Bailey

Bailey alikua nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia majeraha ya goti na inahofiwa huenda fainali za Afrika zikamsababishia matatizo zaidi, endapo atapatwa na dhoruba.

JPM: Kila mtu atabeba msalaba wake
Guardiola: Nakaribia Kustaafu Kufundisha Soka