Mkufunzi wa bondia Manny Pacquiao ambaye ni bondia mkongwe, Freddie Roach amesema kuwa ameamua kupiga chini ombi la Floyd Mayweather aliloliwasilisha kwake alipomtembelea gym hivi karibuni.

Roach alieleza kuwa Floyd ambaye anajiandaa kupambana na bingwa wa Ultimate Fighting Championship (UFC), Conor McGregor alimuomba ajitokeze kumpika mpinzani wake huyo ambaye hana uzoefu katika ulimwengu wa ‘boxing’ bali mchezo wa ngumi na mateke.

“Mayweather alikuja gym kwangu wiki iliyopita na aliomba kukubali kufanya kazi ya kumfundisha Conor McGregor, kwa sababu alinambia pambano hilo lipo na tutatengeneza pesa nyingi,” alisema Roach.

Hata hivyo, alieleza kuwa alilikataa ombi hilo akidai kuwa ili ampike vizuri Conor McGregor kwa ajili ya pambano dhdi ya Floyd inampasa kuchukua sio chini ya miaka mitatu.

Alisema kuwa katika pambano hilo, ni dhahiri kuwa Mayweather atashinda kirahisi kwakuwa ni vigumu kwa mtu anayecheza mchezo wa ngumi na mateke kumpiga mwana masumbwi  bora kama Mayweather katika pambano la masumbwi pekee.

Mayweather na Conor McGregor wanatarajiwa kupambana katika pambano ambalo litawaingizia kiasi kikubwa zaidi cha pesa katika historia ya masubwi.

Bado jicho na masikio ya watu wengi yanasubiri kusikia siku moja Pacquiao na Mayweather wanapanda tena ulingoni kwa pambano la marudiano.

 

Jose Mourinho Ampigia Debe Rio Ferdinand
Serikali yapiga marufuku ‘pombe za viroba’

Comments

comments