Kuelekea mchezo wa marejeano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya Simba dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, kocha wa Simba Patrick Aussems amesema wanajua wanatakiwa kushinda na watafanya hivyo.

Aussems ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari uliohusisha makocha wa timu zote mbili, ambapo mbali na ushindi amesema kikosi chake kipo salama.

“Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo na wachezaji wanajua hilo. Tunatakiwa kuwa makini, tunajua tunakutana na timu nzuri na utakuwa mchezo mgumu lakini tunajiamini”, Patrick Aussems.

Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote katika mchezo huo kutokana na suluhu iliyopata ugenini wiki mbili zilizopita. Mchezo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 10:00 jioni.

 

Maalim Seif akamatwa na Polisi
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 25, 2019