Kocha Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa sasa ndiye Waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Majaliwa amepata nafasi hiyo baada ya kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wingi wa kura za ndiyo baada ya jina lake kuwasilishwa Dodoma na Rais John Pombe Magufuli.

Majaliwa ni mmoja kati ya watu wanaopenda michezo, jambo ambalo lilimfanya asomee ukocha na kupata Leseni B ya Shirikisho la soka Barani Afrika CAF.

Kufuatia kuwa na taaluma hiyo, Majaliwa ana uwezo wa kufundisha timu yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kadhalika Majaliwa aliwahi kufundisha timu mbili zilizowahi kucheza Ligi Kuu ikiwemo Kariakoo ya Lindi na hata Singida United.

Hadi jina lake linapendekezwa na Rais kuwa Waziri mkuu, Majaliwa ni mmoja wa wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lionel Messi Kuvaa Kiatu Hiki Dhidi Ya Real Madrid
Dk Tulia Akson Mwansasu achaguliwa na kuapishwa kuwa Naibu Spika