Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uturuki Fatih Terim, amelituhumu benchi la ufundi la mabingwa wa soka Hispania, FC Barcelona kwa kitendo cha kushindwa kumtumia ipasavyo kiungo Arda Turan.

Terim, ambaye ana jukumu la kukiandaa kikosi cha Uturuki ili kifanikiwe kufanya vyema katika fainali za Euro 2016, amesema hajaridhishwa na maamuzi yaliyofanya dhidi ya kiungo huyo, ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe akitokea Atletico Madrid mwaka 2015.

Amesema Turan ana uwezo mkubwa wa kucheza soka mahala popote na anaamini FC Barcelona wanakila sababu ya kumtumia ipsavyo, lakini akatanabaisha kwamba huenda kukawa na tatizo katika benchi la ufundi la klabu hiyo.

Hata hivyo kocha huyo, ameenda mbali zaidi kwa kuvihusisha vyombo vya habari nchini Hispania kushindwa kumkingia kifua kiungo huyo kwa kusema mapungufu ya benchi la ufundi la FC Barcelona ya kushindwa kumtumia Turan.

Kikosi cha benchi la ufundi la FC Barcelona kinachotuhumiwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uturuki

Amesema katika nchi yoyote duniani vyombo vya habari vimekua na nguvu katika jamii kwa kukataza ama kupongeza juhudi ya jambo fulani, lakini kwa Hispania, Terim anaamini imekua tofauti kwa mchezaji wake.

“Vyombo vya habari vya nchini Hispania navyo havijamtendea haki Arda Turan. Miezi sita amekuwepo FC Barcelona na wanafahamu mchango wake lakini kitendo cha kutokuchezeshwa hakijawahi kuzungumzwa hata siku moja,” alisema Terim.

“Arda ni mzuri katika kila nyanja, tukizungumzia katika ubora kiakili na kimwili. Lakini imekua vigumu kwake kusaidiwa na watu wenye mamlaka ya kuwakumbusha wakuu wa benchi la ufundi la FC Barcelona.

Kabla ya kujiunga na FC Barcelona mwaka 2015, Arda Turan alionekana kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu ya Atletico Madrid, na alikua akicheza karibia kila mchezo uliowahusu wababe hao wa mjini Madrid.

Gonzalo Higuain Amkataa Conte, Amkubali Klopp
Serikali yatahadharisha kukauka mito mikuu, yatenga zaidi ya bilioni 100 kupanda miti