Mara baada ya michoro ya Kodak Black kuondolewa katika makumbusho ya wanamuziki wa HIPHOP nchini Marekani kufuatia kauli aliyoitoa kwa mke wa marehemu Nipsey Hussle ambapo Aprili17, 2019 aliahirisha show aliyotakiwa kuifanya Boston chini Marekani

Kitendo hicho kimewakasirisha mashabiki wake na kujikusanya katika gari lake la ziara ambapo polisi  waliingilia kati baada ya kuonekana kuanzishwa kwa vurugu.

Aidha imeripotiwa kuwa Kodak Black alitarajiwa kutumbuiza kwenye show hiyo ambayo ilipata mahudhurio mazuri lakini hakutokea kwenye ukumbi huo kiasi cha kusababisha vurugu kwa mashabiki ambao walikuwa tayari wamelipa pesa na kuingia ukumbini.

Hata hivyo uongozi wa rapa huyo mtata bado haujatoa sababu  za kuahirisha show yake.

Inadaiwa kuwa rapa huyo kutohudhuria show wengi wamesema kuwa kuwa huenda aliogopa wingi wa watu waliojitokeza na kuhisi kuwa angepigwa au kujeruhiwa kutokana na kauli aliyoitoa kuhusu mke wa Marehemu Nipsey aliposema anamtani.

 

Mjane ajenga nyumba kwa kuuza Uji na Kande kwenye magereji
Mamillioni yamiminika dukani kwa Nipsey Hussle

Comments

comments