Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amezindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la aridhi kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi kupitia Airtel Money.

Uzinduzi wa ulipaji huo mpya wa kodi ya pango la aridhi, unarahisisha huduma hiyo kwani wamiliki wa aridhi wataweza kufanya malipo kupitia simu zao bila kwenda ofisi za wizara ya aridhi.

Akizungumza Jijini Dodoma jana wakati wa kuzindua huduma hiyo, Waziri Lukuvi amesema ubunifu wa Serikali kufanya malipo ya ankara za Serikali kwa kutumia mfumo wa GePG umerahisisha malipo ya tozo mbalimbali za Serikali ikiwemo kodi ya pango la aridhi.

Amesema kuwa mfumo huo wa malipo ya Serikali umekuja na faida nyingi kama vile kutunza kumbukumbu, kulipa kwa muda, kupunguza upotevu wa mapato ya Serikali, kuondoa mwanya wa rushwa na kuongeza mapato ya Serikali.

Waziri Lukuvi amebainisha kuwa lengo la wizara yake kwa sasa ni kutaka kutumia kampuni za simu kuwakumbusha wananchi kulipia kodi ya pango la aridhi kupitia ujumbe wa simu badala ya utaratibu uliopo wa kuwafuata wadaiwa.

” Sasa ofisi za aridhi za kulipia kodi ya pango la aridhi zipo viganjani mwenu, mnaweza kulipa bila kwenda katika ofisi za aridhi” alisema waziri Likuvi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano amesema kuwa wanafahamu umuhimu wa kukusanya kodi na kulipa ya Serikali kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo, pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutumia huduma za kielektroniki kwa kuwa zina ubunifu mkubwa.

Nape amuomba msamaha Rais Magufuli, asema alikuwa halali
Sancho kuikabili Kosovo