Rapa Earl Simmons maarufu kwa jina la DMX, ambaye ni moja kati ya wasanii wakubwa nchini marekani waliopata mafanikio makubwa miaka ya 90, kutokana na mauzo ya albamu yake, hivyo mahakama imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa mwendesha mashaka wa kesi hiyo, DMX anadaiwa kukwepa kulipa kodi kutoka kwenye mapato aliyokuwa akiingiza kuanzia mwaka 2002 hadi 2005, na kutoka 2010 hadi 2015 pamoja na hukumu hiyo bado rapa huyo atatakiwa kulipa dola million 2.29 kwa serikali ya Marekani ikiwa ni sehemu ya deni hilo.

Aidha, muendesha mashtaka wa kesi hiyo amemshutumu rapa huyo kwa kukwepa kulipa kodi na badala yake pesa nyingi alizitumia kufanya matanuzi huku akidai amefilisika.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa DMX kwenda jela, mnamo mwaka 2015 alikaa gerezani kwa miezi sita kwa kosa la kushindwa kulipa pesa ya matumizi ya mtoto wake na mara kadhaa amekuwa akika jela kwa makosa tofauti tofauti ikiwemo kuendesha gari akiwa ametumia kilevi.

CAG awaomba radhi wananchi kuhusu deni la taifa
Viingilio mchezo wa Ngororngoro Heroes dhidi ya Congo DR vyatangazwa