Koffi Olomide ametangaza kuwa amealikwa tena nchini Kenya kutumbuiza kwenye mkutano mkubwa utakaowakutanisha viongozi wa nchi hiyo mwaka huu.

Mwimbaji huyo mkongwe ataizulu Kenya kwa mara ya kwanza tangu alipotimuliwa Aprili 24, 2016 kwa kosa la kumshambulia kwa mateke ‘dansa’ wa kike wa bendi yake.

Kwa mujibu wa tangazo aliloliweka kwenye akaunti ya Twitter, Koffi Olomide anasema mkutano huo wa viongozi wa ngazi za juu utahudhuriwa na viongizi wa kaunti 47 na kwa kawaida huhudhuriwa pia na Rais Uhuru Kenyatta.

Nguli huyo wa rumba mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akiomba radhi mara kwa mara kwa kitendo alichokifanya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Kitendo hicho cha kumpiga teke mfanyakazi wake wa kike kilitafsiriwa kama dharau na ishara ya unyanyasaji wa wanawake akiwa katika ardhi ya kigeni.

Inaonekana Koffi amejifunza na kujutia kitendo hicho, katika video yake anawaambia mashabiki wake wa Kenya, “nimewamiss sana na ninawapenda.”

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 16, 2018
Zari amtukana Diamond, amkumbusha kuhusu watotoÂ