Kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya  Atletico Madrid, Jorge Resurrección Merodio Koke, amesema ilikuwa ni kama katimiza ndoto zake kwa kuichezea timu yake aliyokulia na akasema kuwa timu hiyo itakwenda mbali na kutwaa ubingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Koke alijiunga na Atletico akiwa na umri wa miaka nane na anakumbuka jinsi alivyokuwa akicheza na mchezaji mwenzake, Fernando Torres kabla straika huyo wa timu ya taifa ya Hispania hajahamia Liverpool.

“Watoto wote huwa wanapenda kuwa kama yeye,” Koke aliliambia Shirika la Habari la Hispania (AS). “Tulikuwa tukisema kama utakuwa na nia ya kufanya hivyo, unaweza kufanya.

Tulikuwa wanandoto na ninaona ni bahati imekuwa kweli.”

Tangu alipopangwa kwenye kikosi cha kwanza mwaka 2009, Koke akaonekana aking’ara kucheza nyuma ya washambuliaji kama Sergio Aguero na Diego Forlan na wengine wengi ambapo anasema inakuwa vigumu kwake kuchagua ni mchezaji gani anayevutia.

Hiddink Hajaridhishwa Na Uchezwaji Wa Chelsea
Serikali: Hakuna Viwanja vya Kuwagawia waliobomolewa Mabondeni