Beki wa kati kutoka nchini Ivory Coast na klabu ya Liverpool, Kolo Toure ametishia kuondoka Anfield kama ataendelea kukalia benchi chini ya utawala wa meneja Jurgen Klop.

Toure ambaye ni kaka wa kiungo wa klabu ya Man City Yaya Toure, amesema ni vigumu kwake kuendelea kukaa kwenye klabu ya Liverpool ambayo anashindwa kuitumikia kama ilivyokua matarajio yake.

Beki huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Arsenal na Man City ametishia kufanya hivyo huku mkataba wake ukitarajia kukamilika mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonekana kuhitaji kuendelea kuwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, japo amekua hamtumii mara kwa mara katika mipango yake katika ligi pamoja na kwenye michuano mingine.

“Ni jambo zuri kusikia hivyo kutoka kwa meneja mkubwa (kumbakisha Liverpool),

“Lakini kama nikipata nafasi kwenye kikosi, nitakuwa na furaha zaidi lakini kama sitapata haitakuwa na jinsi,” Toure aliwambia BBC Sport.

Kolo Toure alijiunga na Liverpool mwaka 2013 akitokea Man City ambapo alikabiliwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, hali ambayo ilionyesha kumchosha na kulazimisha kuondoka klabuni hapo mara tu, alipowasili meneja Manuel Pellegrini.

TFF Yamtangaza Afisa Habari Mpya
David Silva Amuweka Njia Panda Manuel Pellegrini