Beki kutoka nchini Ivory Coast, Kolo Toure anaamini hatua ya kujiunga na aliyekua meneja wake akiwa Liverpool, Brendan Rodgers itamuwezesha kuendelea kufikia malengo yake katika soka.

Kolo amejiunga na klabu ya Celtic ya nchini Scotland, baada ya kuthibitishiwa na meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp kutokua na nafasi kwenye kikosi cha The Reds, ambacho alikitumikia tangu mwaka 2013.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 35, amesema ni faraja kubwa sana kwake kufanya kazi kwa mara nyingine tena na Rodgers ambaye alimuamini wakati wote alipokua Liverpool.

“Imenifariji kuona bado nipo katika mikakati yeke, na mimi ninamuahidi sitomuangusha, nipatambana wakati wote ili niweze kufikia malengo yanayokusudiwa hapa” Amesema Kolo.

Brendan Rodgers alimsajili Kolo kwenye klabu ya Liverpool akimtoa Man City kama mchezaji huru mwaka 2013.

Kolo amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya Celtic, na anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake wakati wowote juma hili ambao tayari wameshaanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Kolo amewahi kuitumikia klabu ya Arsenal na kisha alijiunga na Man City klabla ya kwenda Liverpool.

Amefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini England mara mbili akiwa na klabu za Arsenal na Man City, kombe la FA mara tatu (Arsenal mara mbili) na Man City mara moja.

Ngao ya jamii mara tatu, Arsenal mara mbili na Man City mara moja.

Game Ya Man Utd Vs Man City Yapigwa Kalenda
Hakuna Kanuni za kukagua Wimbo Kabla ya Kuachiwa- Roma