Wataalam wa teknolojia wamegundua njia ambayo inaweza kuwa mwarubaini wa watu kutopoteza vitu vyao kirahisi kwa kuvibaini popote vilipo kwa kutumia simu za kisasa (Smartphone).

Teknolojia mpya iliyopewa jina la TrackR itawasaidia zaidi watu wengi waliokuwa wanashindwa kujiunga na huduma mbalimbali za kuwekea ulinzi vyombo vyao vya usafiri (track) ili kubaini vilipo, kwa kuzingatia kuwa mtu huhitaji kulipia gharama za kila mwezi kwa huduma hiyo inayotolewa na makampuni mbalimbali yanayotumia mfumo wa ‘GPS’.

Kampuni moja imebuni kifaa kinachofahamika kama Track R kinachouzwa kwa bei ambayo watu wengi wenye uchumi wa chini wanaweza kununua, kinachounganishwa na simu ya kisasa ya mtumiaji husika.

Mtumiaji anapaswa kufunga kifaa hicho kidogo kwenye kitu anachotaka, kisha ata-download application ya ‘Track R’ kwenye simu yake ya mkononi ya (iPhone au Smartphone) na kuiunganisha na kifaa hicho.

Baada ya kukamilisha utaratibu huo, simu yake itakuwa na uwezo wa kumueleza mahali popote kilipo kitu hicho.

Tofauti na mfumo ule uliokuwa umezoeleka, hapa mteja hatakuwa na haja ya kulilipia gharama za kila mwezi kwa huduma hii.

Kifaa hicho kidogo kinaweza kuwekwa pia kwenye vitu kama mabegi, pochi, mikoba na vitu vingine kwa kuficha ndani yake.
Angalia maelekezo hapa:

Nikitakiwa na WCB Ntakubali Nataka Kufika Mbali- Young Killer
Video: BAWATA Wamekuja na Haya Tena Kuhusu Matatibu Waliofutiwa Usajili