Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong – un amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa tayari kutumia mabomu ya nuclear muda wowote.

Kwa mujini wa taarifa zilizotolewa na chombo cha habari cha taifa hilo, Kim Jong-un aliwaambia viongozi wa jeshi kuwa nchi hiyo inapaswa kuwa tayari kufanya mashambulizi ya ki-nuclear kwa taifa lolote, kabla haijashambuliwa.

Jumatano, Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza kuiwekea nchi hiyo vikwazo vizito zaidi kuwahi kutokea, kufuatia hatua za majaribiko ya mabomu ya nuclear yaliyofanywa na nchi hiyo hivi karibuni.

Rais Museveni afikishwa mahakamani
Magufuli ahamishia kasi ya ujenzi Afrika Mashariki, asema Wananchi hawahitaji ‘mavyama’