Korea kaskazini na kusini wamekubaliana kuandamana pamoja chini ya bendera moja ya ‘ushirikiano wa Umoja waKorea’ mwezi ujao katika mashindano ya Olympiki ya majira ya baridi yanayotarajiwa kufanyika Korea ya kusini.

Pia nchi hizo mbili zimekubaliana kuungana katika timu ya wanawake ya mchezo wa magongo (Hockey) kufuatia mazungumzo adimu yaliyofanyika katika Kijiji cha Panmunjom.

Mazungumzo hayo ni ya kwanza kwa ngazi za juu kukutana kati ya nchi hizo mbili za Korea baada ya kushindikana miaka miwili iliyopita.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Februari 9 hadi 25 katika mji wa Pyeongchang nchini Korea ya Kusini.

Iwapo mipango hiyo itakubalika mamia ya viongozi, mashabiki na wanamuziki na wachezaji wanatarajiwa kuvuka mpaka wa Korea Kusini kwaajili ya kushuhudia michezo hiyo.

Viongozi Chadema watiwa mbaroni kuhusika na tukio la moto
Serikali yazifutia usajili meli zilizopeperusha bendera ya Tanzania