Pamoja na kwamba Mataifa mbali mbali yanakemea majaribio ya makombora ya Nyuklia yanayofanya na nchi ya Korea Kaskazini, nchi hiyo imesema kuwa itaendelea zaidi kufanya majaribio ya makombora yake kila juma, kila mwezi na kila mwaka.

Hayo yameelezwa na Waziri wa masuala ya kigeni, Han Song-ryol wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Pyongyang

”Tutafanyaa majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma, kila mwezi na kila mwaka,” amesema waziri huyo

Aidha, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence ameionya Korea kutoichokoza Marekani, amesema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha na sasa Marekani haitakuwa na subira tena dhidi ya Korea Kaskazini.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma muda huu
Video: Polisi kimya kimya, Ubadhirifu wa kutisha NIDA

Comments

comments