Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amekamilisha mchakato wa kupitia mpango wa kufyatua makombora manne kuelekea katika ardhi ya Guam ya Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya uamuzi huo iliyochapishwa na chombo cha habari cha taifa cha nchi hiyo, KCNA, Kim Jong Un amesema kuwa wameamua kutulia wakisubiri kuona Marekani itafanya nini kwanza.

Kauli hiyo ya Kim Jong Un imekuja baada ya Katibu wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis kueleza kuwa kama Korea Kaskazini itathubutu kuishambulia ardhi yoyote ya Marekani basi ‘mchezo utakuwa umeanza rasmi’.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani, Mattis aliwaambia waandishi wa habari, “hauwezi kuwashambulia watu katika dunia hii isipokuwa unataka kubeba madhara ya vitendo vyako.”

Kwa mujibu wa KCNA, Kim Jong Un ameshaufanyia usaili mpango wa kushambulia Guam kwa muda mrefu na kwamba ameendelea kujadiliana na wataalam wa jeshi la nchi yake.

Rais wa Marekani, Donald Trump amewahi kukaririwa akimuonya Kim Jong Un kuwa akijaribu kuishambulia Marekani atashuhudia vitendo vya ‘kipuuzi’ vya Wamarekani dhidi ya nchi yake.

Marekani na Korea Kaskazini wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kufanya majaribio ya mabomu ya kinyuklia.

Korea Kusini ambayo ni hasimu wa Korea Kaskazini, imesisitiza kuwa nchi yoyote inayotaka kuishambulia Korea Kaskazini ni lazima ifanye makubaliano nayo kuhusu mpango huo.

Prof. Lipumba amtaka Maalim wayamalize, awapiga dongo Chadema
Serikali yalipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)