Korea Kusini imependekeza kufanyika kwa mazungumzo na Korea Kaskazini, ili kuweza kutatua tofauti iliyojitokeza kati ya nchi hizo mbili kitu ambacho kilipelekea Korea Kaskazini kufanya majaribio kadhaa ya silaha za nyuklia.

Katika mazungumzo hayo ambayo yanatarajiwa kuwa ni ya kwanza tangu mwaka 2o15 kufanyika ambapo yatalenga kutatua misukosuko iliyojitokeza baina ya nchi hizo mbili jirani ambazo zimekuwa katika mzozano.

Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in ameonyesha tangu mwanzo kutafutia ufumbuzi wa kidiplomasia ili kuwepo na ushirikiano wa karibu na Korea ya Kaskazini na kuondoa tofauti zilizopo.

Aidha, hivi karibuni akitoa hotuba yake mjini Berlin, alisema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka muafaka kuafikiwa ili kuweza kuondoa tofauti baina yao.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.

Video: Nitagombea urais tena mwaka 2020 - Lowassa, Mitambo IPTL yazimwa
Uwanja wa mpira wabomoka na kuua wanane wakati wa vurugu za mashabiki

Comments

comments