Serikali ya Korea imepanga kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu kwa kuwaleta walimu nchini walimu wa masomo ya hisabati na Sayansi ili kusaidia kupunguza uhaba wa walimu hao.

Rais wa Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (NIIED), Kim Kwang -Ho kutoka Korea, alisema kuwa nchi yake imekuwa ikisambaza walimu kwa nchi zinazoendelea na kwamba hadi sasa imeshasambaza walimu 61 katika nchi hizo. Aliyasema hayo jana alipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema katika mpango huo, mwaka huu imepanga kusambaza walimu 140 kwa nchi 15 na Tanzania ni moja kati ya nchi hizo na itapata walimu watano wa somo la hisabati na watano wa masomo ya Sayansi (jumla walimu 10).

“Tumeona katika kuunga mkono juhudi za serikali kuongeza walimu wa masomo ya sayansi na kwa mara ya kwanza mwaka huu taasisi yetu itasambaza walimu 10 hapa Tanzania kati yao watano watahusika katika masomo ya hisabati na wengine watano watahusika na masomo ya Sayansi,” Kwang-Ho anakaririwa.

Kadhalika, alisema kuwa Serikali ya nchi yake inatoa ufadhili kwa wanafunzi wenye vipaji ili kuendeleza masomo yao katika taasisi za elimu ya juu kwa lengo la kuwasaidia kukuza viongozi wa baadae wenye elimu.

 

Tyson Fury Atamba Kwa Umbile Lake
Magaidi wapanga kumteka Manny Pacquiao, Rais Wa Ufilipino anena