Korea Kaskazini imeendelea na utaratibu wake unaopingwa na Marekani wa kufanya majaribio ya silaha za nyuklia ambapo leo imefanya jaribio lingine la silaha za aina hiyo huku ikisisitiza kutoacha mpango wake huo.

Aidha, Jaribio hilo limefanyika wiki moja baada ya nchi hiyo kulifanyia majaribio kombora lingine ambalo ilidai kuwa ni jipya na ambalo lina uwezo wa kubeba silaha kubwa za nyuklia.

Katika kikao cha dharula cha baraza la umoja wa mataifa kilichofanyika Jumatatu iliyopita baraza hilo liliitaka Korea Kaskazinia kusitisha mara moja mpango wake huo wa kufanya majaribio kama hayo.

Hata hivyo, Korea Kaskania inafahamika kwa kutengeneza zana za nyuklia na imefanya jumla ya majaribio matano ya nyuklia na ya makombora yenye uwezo wa mkubwa wa kusafirisha zana hizo hadi maeneo inayolenga.

 

Serengeti boys kupambana na Niger leo
Klabu ya Arsenal hati hati kupigwa mnada