Serikali imeruhusu korosho inayonunuliwa na wafanyabiashara katika msimu huu wa 2021/22 kusafirishwa katika bandari ya Dar es Salaam, Mtwara.

Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe ametangaza uamuzi huo wa serikali mapema leo Jumapili Oktoba 31, 2021.

“Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uamuzi huo baada ya kusikiliza maoni ya wafanyabiashara kufuatia changamoto kubwa ya upatikanaji wa makasha na meli unaoikumba dunia kwa sasa na kupanda kwa gharama za usafirishaji kwa njia ya bahari,” amesema Bashe.

Bashe amesema gharama za kusafirisha tani moja ya korosho kwa kutumia bandari ya Mtwara sasa hivi ni dola za Marekani 120 hadi 180 kutegemeana na aina ya meli mfanyabiashara anayotumiwa ya makasha (container vessel) au ya kichele (bulk cargo vessel) ambayo ni ongezeko la zaidi ya dola za kimarekani 100 katika bandari ya Dar es Salaam.

Aidha amewaambia wafanyabiashara kuwa bei ya korosho duniani haijaanguka, ambapo amesema kuwa kwa kurusu bandari ya Dar es Salaam kutumika ni kutokana na gharama za usafiri na upatikanaji wa makasha ni nzuri zaidi kuliko bandari ya mtwara.

Ulaji wa njegere unavyosaidia kuto zeeka haraka
Jay-Z sasa ni Hall of Fame