Umoja wa Mataifa UN, umezindua kozi mpya ya mtandaoni inayowapa watumiaji wa jukwaa la wikiHow la vidokezo muhimu kuhusu jinsi ya kujilinda na taarifa potofu na hatari, ambazo zinazidi kujaza majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo inakuja kufuatia uwingi wa makala zinazopotosha au taarifa za ulaghai zinavyoendelea kujitokeza katika rekodi za matukio na mijadala ya habari, huku kozi hiyo ikitarajiwa kuwasaidia watumiaji kuchambua na kutenganisha vitu halisi na visivyo ikiwemo kuzuia kueneza uzushi.

Muonekano wa ‘App’ mbalimbali za simu. Picha ya Mtandao.

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2020, ulioidhinishwa wa kuboresha ufikiaji wa taarifa sahihi mtandaoni na wikiHow, umekuwa ukishirikiana na wadau, ili kuwasaidia watumiaji kuwa salama dhidi ya taarifa za upotoshaji na habari zisizo sahihi.

Katika sasisho lake la hivi karibuni, wikiHow imethibitishwa inasaidia watumiaji kutambua maudhui ambayo si sahihi, yaliyoundwa kimakusudi, ili kudanganya na kusababisha madhara au kuzua taharuki kwa watumiaji wa mitandao.

Serikali yataka mabadiliko ukuzaji sekta ya uzalishaji
Wenye ukoma wataka kutambuliwa kimataifa