Mbunge wa Ubungo, aliyemaliza muda wake, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya CHADEMA na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo leo na kupokelewa na Mwenyekiti Maalim Seif Sharif Hamad.

Kubenea amesema “Nimekuwa kwenye harakati za kutetea mfumo wa vyama vingi, haki sawa kwa watu wote, haki za kisheria, haki za binadamu kwa karibu miaka 20 sasa. Nimekuwa Mbunge wa Ubungo kwa miaka mitano”.

Na kuongeza, “Nimelazimika kuondoka huko nilikokuwa. Nawashukuru sana viongozi wakuu bila kuwataja majina waliofanikisha mimi kufika leo. Uamuzi huu haukuwa mwepesi, ulikuwa mgumu sana kwa sababu katika maisha yangu, hiki ndicho chama cha pili kujiunga”.

Pia, katika hafla hiyo, zaidi ya wanachama 48 wa CHADEMA wamejiunga na ACT-Wazalendo.

Waziri Mkuu ahimiza kilimo cha mboga Ruangwa
Rais Magufuli ameahirisha sherehe za Mashujaa