Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amekanusha taarifa ya kufukuzwa katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Amesema kuwa hajafukuzwa bali walitakiwa kuhama na kuelekea Halmashauri ya Ubungo hivyo walishakabidhi ofisi hizo zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Aidha, amesema kuwa yeye ameamua kupanga nyumba ili kuweza kuwahudumia wananchi na wapiga kura wake wa jimbo la Ubungo.

“Mimi sikufukuzwa niliondoka mimi mwenyewe kulingana na taratibu zilizopo, hivyo mkuu wa wilaya ya Kinondoni kusema kuwa katufukuza sio za kweli,”amesema Kubenea.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za kufukuzwa ofisini kwa wabunge wa Chadema waliokuwa wakitumia ofisi zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Mmiliki wa shule ya 'daycare' ahukumiwa jela miaka 21
Ndege ya Bangladeshi yalipuka na kuua 50

Comments

comments