Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ameifikishwa mbele ya ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Wilbroad Mashauri akikabiliwa na tuhuma za kuandika na kuchapisha habari za uongo kuhusu Zanzibar.

Akisoma mashtaka dhidi ya mbunge huyo jana, Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi alisema kuwa mshtakiwa aliandika habari za uongo ambazo zingeweza kuleta hofu kwa jamii kupitia gazeti la Mwanahalisi toleo la Julai 25 -31 mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar’.

Wakili huyo wa Serikali aliieleza Mahakama kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo tayari umekamilika na wako tayari kuendelea na hatua nyingine za kesi hiyo. Hata hivyo, Kubenea alikana mashtaka yote dhidi yake.

Watafiti nchini wagundua programu ya kuchunguza saratani ya kizazi kwa simu
TCRA yafungia Kipindi cha Clouds TV kwa kuhamasisha ukahaba