Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imewashushia rungu la kuwasimamisha wabunge wa Upinzani, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Tundu Lissu, Esther Bulaya, John Heche, Godbless Lema na Paulina Galuk kwa makosa yaliyotokana na matendo yao walipodai kurushwa moja kwa moja kwa vikao vya Bunge kupitia TBC1.

Taarifa ya Kamati hiyo imeeleza kuwa wabunge hao kwa njia tofauti walichangia katika kutokea kwa vurugu bungeni, Januari 27 mwaka huu na kushindwa kuheshimu maamuzi na maelekezo ya Spika/Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume cha kanuni na taratibu za Bunge hilo.

Zitto Kabwe na Halima Mdee ni kati ya waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Septemba mwaka huu. Adhabu hiyo pia imewashukia lema na Geluk.

Heche ameamriwa kutoshiriki vikao 10 vya Bunge hilo.

Bunge

Zlatan Ibrahimovic Awachanganya Wadau Wa Soka Duniani
Aliyekuwa Katibu Mtendaji TCU aunga mkono kutumbuliwa kwake