Historia inaweza ikawa inawabeba sana Argentina kuelekea mchezo wao wa fainali dhidi ya Brazil kunako COPA AMERICA lakini lolote kwenye mchezo wa soka linaweza kutokea.

Takwimu zinatuambia wameshakutana mara 33, Argentina kashinda mechi 13, Brazil mechi 10 wameenda sare 8.

Kwangu ni mechi itakayoamuliwa zaidi na hawa viumbe wawili. Huku Messi kule Neymar, kwenye mashindano haya ya mwaka huu wamekuwa katika viwango bora sana.

Mchezo utafanyika kunako Dimba la Maracana katika Jiji la Rio de Janeiro nchini Brazil.

Kutokana na mlipuko wa COVID-19 unaoendelea kuisumbua Dunia, 10% tu ya mashabiki ndiyo watakaoruhusiwa kushuhudia mchezo huu Live kutoka uwanjani.

Wote ni lazima wapimwe na wawe salama. Sio mbaya, hapa zege halilali.

Mechi itachezwa saa 9 kamili alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki. Usiku wa kuamkia Jumapili ya Julai 11, 2021.

Brazil yupo nyumbani, atahitaji heshima ibaki kwake. Argentina yupo ugenini, naye atataka kuweka rekodi yake.

Tatizo la Brazil kwa miaka ya hivi karibuni hawajawa na matokeo mazuri sana wakiwa katika ardhi ya nyumbani hususani pale inapofika katika hatua hizi kubwa za mwisho.

Utakumbuka nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014, waliambulia kichapo kikali cha 7-1 kutoka kwa Ujerumani.

Imeandaliwa na Jackson Sillo

Serikali imetenga Bilioni 1 ujenzi Taasisi ya Sayansi ya Bahari
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 10, 2021