Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetoa, maelezo ya upangaji wa makundi kuelekea kwenye fainali za mataifa ya barani humo za mwaka 2016 ambazo zitafanyika nchini Ufaransa.

UEFA wametangaza utaratibu huo, huku zikisalia timu nne, kuingia kwenye mlolongo wa timu zitakazoshiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya, ambazo zitacheza michezo ya hatua ya mtoano.

Mpaka sasa mataifa 20 ndio, yamefanikiwa kutinga kwenye fainali hizo baada ya kufuzu kwenye hataua ya makundi.

Maelezo ya upangaji wa makundi ya fainali za mwaka 2016 ambapo hafla yake itafanyika Disemba 12 jijini Paris nchini Ufaransa, yanaonyesha timu ya taifa ya England, imewekwa katika chungu cha kwanza sambamba na mataifa ya Hispania, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji pamoja na Ureno.

Chungu cha pili kitakua na timu za taifa ya Italia, Urusi, Uswiz, Austria pamoja na Croatia.

Chungu cha tatu kitakua na timu za Poland, Romania, Slovakia huku timu nyingine mbili zikitarajia kupatikana baada ya michezo ya hatua ya mtoano ambayo itachezwa mwezi novemba.

Chungu cha nne kitakua na timu za Wales, Iceland, Ireland ya kaskazini pamoja na Albania huku timu nyingine mbili zikitarajiwa kupatikana baada ya michezo ya mtoano mwezi ujao.

Chungu kingine kitakua na timu za mataifa ya jamuhuri ya Czech, Uturuki pamoja na mataifa mengine ambayo yanasubiri kupenya katika michezo ya hatua ya mtoano.

Ikumbukwe kwamba bingwa mtetezi wa fainali za mataifa ya barani Ulaya ni timu ya taifa ya Hispania.

Mkwasa: Algeria Ni Kihunzi Kikubwa
Luka Modric Kuikosa Levante