Hapa karibuni matukio ya Basata pamoja na wasanii yamekuwa yakichukua nafasi kubwa. Wapo wasanii mbali mbali waliokutwa na changamoto ya kufunguiwa video za wimbo au wimbo wenyewe (audio). Mwanamuziki Shaa alishawahi kuwa muhanga wa kufungiwa kazi zake na Basata.

Shaa anasema kufungiwa kwa nyimbo kunamrudisha nyuma msanii kutokana na kwamba msanii anawekeza pesa na muda katika uandaaji,ikitokea kuwa umefungiwa video pamoja na audio lazima ikuume kwani muziki huo ndio kazi yako pia ni biashara.

“Hii ni kazi, hii ni biashara, ni sawa kwa mfano mimi nina perfume yangu hii hapa, nimewekeza hela halafu ikafungiwa, mtu hawezi kujua ni kitu gani, siwezi kuipost, siwezi kuitangaza, kwahiyo hiyo hela inakuwa imepotea.”- Shaa.

Kutokana na Basata kuwa macho kutazama suala la maadili katika kazi za wasanii kumemfanya Shaa kurudisha kazi yake kwa Justin Campos ili aweze kufanya marekebisho ya video yake mpya ya ‘Sawa’.

”Sitaki kosa hili lijirudie kama ilivyofungiwa video ya sugua gaga,napenda kazi zangu zote zionekane audio na video kwa pamoja ndio maana nmeamua kurudi kufanya marekebisho kabla haijatoka”. Shaa aliiambia bongo5.

Shaa ‘Malkia wa uswazi’ alishawahi kukutwa na mkasa wa kufungiwa video ya wimbo wake wa sugua gaga huku wimbo wake wa Toba ukipewa masharti ya kuchezwa usiku katika runinga aidha wahanga wengine wa kufuli la basata ni Snura, Jux, Nay wa Mitego na Wasanii wengine.

FA Yafanya Mabadiliko Ya Sheria Za Ligi Kuu
Giuseppe Marotta: Hakuna Makubaliano Yoyote Kuhusu Pogba