Msanii wa Bongo fleva Diamond Platinumz amefunguka sababu ya ndoa yake kusogezwa mbele akidai kuwa ndoa hiyo inatarajiwa kuwa ni moja ya ndoa kubwa zitazowahi kufungwa hapa nchini na kusema kuwa itakuwa ni ndoa ya kifalme na kuifananisha na ile iliyofungwa na Prince William mjukuu wa Malkia Elizabeth.

”Watu wengi wanatakiwa kuhudhuria, sababu ndoa yangu watakuja kina Rick Ross, Omarion, ”I want it to be a royal wedding kama unavyoona wale Prince wa uingereza zilivyokuwa” amesema Diamond.

Diamond anatarajia kufunga ndoa na mtangazaji wa radio ya RNG, iliyopo huko nchini Kenya, Tanasha Dona ambaye alipohojiwa alijitapa na kusema kuwa ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa kwa muda wa siku nne hivyo watu wasitarajie  wawili hao kuachana.

Ndoa hiyo imepelekwa mbele na ilitarajiwa kufanyika tarehe 14 Febuari katika siku ya wapendanao siku ambayo ilileta gumzo mwaka jana hasa kwa wadau wa masuala ya burudani na wafuatiliaji wakubwa wa mahusiano ya msanii Diamond ambapo mama watoto wake Zarinah Hassan rasmi alivunja mahusiano yao.

Aidha mashabiki na watu wa karibu wa wasanii hao wanapatwa wasiwasi mkubwa juu ya uwepo wa ndoa hiyo kwani kumekuwa na panga pangua za hapa na pale ambazo zimewafanya hali inayopelekea wadhani kuwa matambo yote juu ya harusi hiyo ni kiki.

 

 

Ajinyonga na kuacha ujumbe mzito
Video: Rais Magufuli ateua viongozi hawa leo