Uamuzi wa Rais John Magufuli kufuta sherehe za maadhimisho ya siku yaUkimwi duniani, Disemba 1 kumepokelewa kwa mtazamo chanya na watu wengi huku wengine wakilia kuwa umewasababishia hasara.

Wajasiriamali ambao wamefika katika mji wa Singida tayari kwa kushiriki maadhimisho hayo wamelalamika kuwa wamepata hasara kutokana na uamuzi huo kutolewa ndani ya muda mfupi.

Wameeleza kuwa wameingia hasara ya maandalizi, gharama za kukaa katika mji huo pamoja na nauli huku wengine wakidai kuwa hawafahamu wataweza vipi kurejea makwao kwani walitegemea faida watakayoipata kwa kuuza madawa ya tiba asilia.

Hata hivyo, wajasiriamali hao walimpongeza rais kwa uamuzi waliochukuwa kwani utasaidia zaidi kuongeza madawa ya kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV).

“Hatua ya Rais ni nzuri kwa sababu dawa zitapatikana kwa wingi hospitalini, lakini ametushtukiza mno. Angesema mapema tusije kabisa huku Singida,” alisema Hussein Singu.

Rais Magufuli alitoa amri ya kutofanyika sherehe katika siku ya Ukimwi duniani mwaka huu na badala yake bajeti yake ipelekwe katika kununua ARV.

Utoaji elimu na kupima kwa hiari utaendelea kama ilivyokuwa kwa miaka mingine lakini hakutakuwa na hotuba, risala na kongamano.

Diamond: Sitaki kabisa kushika simu ya Zari, namjua...!
Millard Ayo Aeleza Alivyowahi kudata Kimapenzi Kwa Jokate