Kituo cha Haki Za Binadamu (LHRC) kimetoa tamko rasmi kufuatiwa kukamatwa kwa watumishi wake Oktoba 29 baada ya polisi kukizingira kituo hicho na kupekua kisha kukamata computers na simu zote za wafanyakazi hao.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kitaifa wa kituo hicho, Onesmo Olenguruma alithibitisha kukamatwa kwa wafanyakazi hao na kueleza kuwa ingawa walifikishwa katika kituo cha polisi na kutolewa kwa dhamana baadaye, walipowasiliana na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi hilo walionesha kutolifahamu tukio hilo.

“Baada ya kuzipata taarifa hizo, sisi kama mtandao tulifanya jitihada za kuwasiliana na jeshi la polisi ofisi ya IGP na baadae ofisi ya Oparesheni kwa Chagonja, na baadaye kwa Ofisi ya Afisa Upelelezi Kanda pale kwa Masawe, kwa ajili ya kujua nini kimetoa na kwanini. Lakini inaonekana kuwa hata wao Jeshi la Polisi ngazi za juu hawakuwa na taarifa hizo,” alisema Olengurumo.

Mratibu hiyo alieleza kuwa wafanyakazi wake walikuwa wanaendelea na kazi za kisheria wakati huo na sio vinginevyo. Alisema wafanyakazi hao walifikishwa mahakamani ambapo walikana mashitaka na kupewa dhamana.

Mratibu huyo alivitaja vifaa vilivyokamatwa na kuchukuliwa na Jeshi la Polisi katika tukio hilo.

“Vifaa vyote vya kutendea kazi pamoja na vifaa binafsi vilichukuliwa katika kituo hicho ambavyo ni computer mpakato 2, computer za mezani 26 na simu za mkononi wafanyakazi zote 36 pamoja na simu za kazi walizokuwa wanazitumia.”

Taarifa za awali zilidai kuwa polisi walivamia kituo hicho na kuchukua vifaa hivyo pamoja na watumishi hao kwa tuhuma za kujihusisha na zoezi la kufanya majumuisho ya kura kinyume cha taratibu za uchaguzi.

NEC Yarudi, Yafafanua Kuhusu Idadi ya Wapiga Kura Kutofautiana Na Waliyotangaza
Sikio la Baba Na Mama Izzo Bizness ni Chanzo cha Tunayoyasikia