Maofisa wa bustani moja nchini Ufaransa, wamesema wanatarajia kutumia kunguru sita kukusanya taka na kusafisha eneo hilo, baada ya kupewa mafunzo maalum.

Kwa mujibu wa maofisa hao, kunguru hao  waliopo katika bustani ya  Puy du Fou theme park, iliyopo  Magharibi mwa nchi hiyo wamefunzwa kukusanya mabaki ya sigara na taka nyingine ndogo ndogo.

Walisema kunguru wa kwanza tayari wameanza kufanya kazi huku wengine wakitarajiwa kujiunga nao leo.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kunguru kuonesha uelewa wao, baada ya  mapema mwaka huu wanasayansi  kuunda mashine ambayo ilioneesha uwezo wa  viumbe hao kutatua masuala Fulani kwa kutumia ukubwa wa karatasi.

Katika utafiti huo, wanasayansi  hao waligundua kuwa kunguru wanaweza kukumbuka ukubwa wa karatasi hiyo na hata wangeikata na kuipindua kama haingeweza kutosha kwenye mashine.

Samsung kuzindua 'memory Card' ya 512 GB
Majaliwa awataka viongozi wabadilike kimtazamo

Comments

comments