Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho alimtukana tusi kubwa Daktari wa klabu hiyo, Eva Carneiro.

Video iliochiwa na Sky Sports imeonesha Mourinho alivyomchukia na kumtukana Eva kwa maneno ya kireno ‘filho da puta’ (ambayo tafsiri yake ni mtoto wa mbwa).

Chanzo cha Mourinho kumtukana Carneiro ni kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard wakati wa dakika za majeruhi za mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Swansea ambayo walitoka sare ya 2-2 uwanja wa Stamford Bridge .

Sportsmail nao wanasema wachezaji wa Chelsea wameduwaa na maneno makali ambayo Mourinho anabwatukajuu yao na viongozi wengine wa timu.

Mourinho leo anakutana na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu amtukane Carneiro na kumfungia kukaa kwenye bechi katika mechi zijazo.

Comments

comments