Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania lilikumbwa na msiba mkubwa mara baada ya kupoteza roho za watanzania zaidi ya 1000 katika ajali mbaya ya Meli ya MV Bukoba iliyozama hatua chache takribani kilomita 30 kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea Mkoani Kagera.

Leo Mei 21, 2018  ni kumbukumbu ya miaka 22 tangu kutokea kwa ajali hiyo mbaya ambapo viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali na kufanya kumbukumbu.

Katika ajali hiyo ripoti iliyotolewa ilieleza kuwa watu 114 waliokolewa wakiwa hai, huku watu 391 waliopolewa wakiwa wamefadriki dunia na miili 332 haikupatikana.

Ambapo miili iliyoopolewa ikiwa imefariki Serikali iliamua kuizika katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma nje kidogo ya jiji la Mwanza na miili mingine kuchukuliwa na kuzikwa na ndugu katika maeneo yao.

Miss Universe Tanzania 2007 mwanamitindo wa kimataifa anayeiwakilisha vyema Tanzania, Flaviana Matata anaikumbuka siku hiyo kutokana na kumpoteza mama yake mzazi na kaka yake waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika,

”It has bee 22 years since we lost our dears ones including my Mom in the most human tragedy, Mv Bikoba sinking May their souls continue to Rest in Peace.

Akimaanisha Miaka 22 sasa imepeita tangu tuwapoteze wapendwa wetu akiwemo mama yangu mzazi katika ajali mbaya ya kuzama kwa Meli y Mv Bukoba, Nazitakia roho zao ziendelee kupumzika kwa amani.

Ni moja kati ya majanga makubwa ambayo Watanzania waliyapitia hakika tutaendelea kuikumbuka siku hii na kuendelea kuziombea roho zote za marehemu zilizopotea katika ajali ya Mv Bukoba.

Aidha meli ya MV Bukoba iliundwa mwaka 1979 na kufanya kazi kwa miaka 17 tangu anguko lake, ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 430 na mizigo yanye tani 850 na siku iliyozama ilikuwa imebeba abiria 800 na wafanyakazi 37.

 

Chanjo ya Ebola yaanza kutolewa nchini Congo DR
Polisi wapigwa marufuku kula hadharani, kuweka mikono mfukoni