Viongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) akiwemo Mwenyekiti wake, Patrobas Katambi wamekamatwa na jeshi la polisi jana usiku mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya BAVICHA kutangaza mpango wao wa kwenda mjini humo kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano mkuu wa CCM, utakaowezesha Rais John Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa chama hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa viongozi hao wa BAVICHA na kueleza kuwa wanatuhumiwa kwa kukusudia kuhamasisha vurugu na kuikashifu serikali. Amesema kuwa viongozi hao hawatapata dhamana hadi Jumatatu ijayo watakapofikishwa mahakamani.

Naye Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema –Taifa, Joseph Kasambala ameliambia gazeti la Mwanahalisi kuwa viongozi waliokamatwa ni pamoja na Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Julius Mwita, Katibu wa Bavicha -Taifa na George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya.

Kasambala amesema kuwa taarifa walizozipata katika kituo hicho cha polisi, viongozi hao wanatuhumiwa kuikashifu serikali, kwa kuvaa fulana zenye maandishi “Dikteta Uchwara”.

Lowassa afunguka kuhusu hali ya Siasa nchini, awapa Chadema ‘ukweli mchungu’
Polisi waukingia kifua mkutano wa CCM, 'hakuna marufuku juu ya mikutano hiyo'